Language

Friday 25 January 2013

HABARI: JESHI KUCHUKUA UONGOZI UGANDA?

Baada ya sakata la kufariki ghafla mbunge wa chama tawala NRM nchini Uganda,rais Museveni pamoja na waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi wamekuwa wakitoa kauli za kutishia kuliachia jeshi lichukue uongozi nchini humo. 

Nchini Uganda baada ya sakata la wiki kadhaa la kufariki ghafla mbunge wa chama tawala NRM na aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya chama chake inayoongozwa na Museveni Selina Nambanda,sasa rais pamoja na waziri wa ulinzi na mkuu wa majeshi katika nyakati tofauti wamekuwa wakitoa kauli za kutishia kuliachia jeshi lichukue uongozi nchini Uganda. Yote yanatokana na mpasuko ndani ya chama cha NRM ambapo wabunge wa chama hicho wamekuwa wakitaka ianzishwe tume huru ya kuchuguza kifo hicho,hatua ambayo inapingwa na rais Museveni.Wabunge kadhaa wameshatiwa ndani kufuatia hoja hiyo.Kinachowatia wengi mashaka kwa sasa ni kauli hizo za kutaka jeshi liidhibiti serikali, Saumu Mwasimba amemuuliza mchambuzi wa masuala ya kiasiasa,mhadhiri wa masuala ya sheria katika chuo kikuu cha Makerere,Dkt John Nsokwa anaitazama vipi hatua hii. Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...