Language

Wednesday 27 March 2013

BANDA AKANUSHA MASHTAKA


Rais wa zamani wa Zambia Rupiah Banda amesema hana hatia katika kesi anayokabiliwa nayo ya kutumia vibaya mamlaka wakati wa kipindi chake cha uongozi.

Mashtaka anayokabiliwa nayo Banda yamehusishwa na mkataba alioidhinisha kati ya nchi hiyo na Nigeria kuhusu uuzaji wa mafuta ambao wendesha mashtaka wanasema ulinuia kufaidi bwana Banda na familia yake.
"hapana bwana Jaji , nakanusha mashtaka ,'' Banda alimbia jaji.

Rais huyo wa zamani anasema kuwa mashtaka hayo ni sehemu ya njama za kisiasa dhidi yake na washirika wake.
Baada ya miaka mitatu mamlakani, alishindwa na mpinzani wake Michael Sata katika uchaguzi mwaka 2011, ingawa aliachiliwa kwa dhamana siku ya Jumatatu.
Wendesha mashtaka wanasema kuwa Banda na mwanawe Henry Banda waliweka pesa katika akaunti za kigeni, pesa zilizotokana na mkataba wa mafuta kati ya Zambia na Nigeria. Pesa hizo inadaiwa zilitumika kufaidi familia ya Banda.
Henry Banda aliondoka nchini baada ya babake kushindwa kwenye uchaguzi na anasakwa na polisi.
Serikali ya Sata imeanzisha uchunguzi dhidi ya washirika wakuu wa Banda kufuatia madai ya kuhusika na ufisadi wakati wa utawala wa Banda.
Waziri mmoja wa zamani amepatikana na hatia na anajiandaa kukata rufaa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...