Language

Wednesday 27 March 2013

WAFANYA KAZI ZA NYUMBANI SASA KUPATA HAKI ZOTE BRAZIL


Baraza la Senate nchini Brazil, limepitisha bila pingamizi, mswaada wa kihistoria unaowapa haki sawa wafanyakazi wa majumbani na wale na maofisini kote nchini.

Sheria hiyo mpya, inafafanua idadi ya siku za kazi ambazo wafanyakazi hao pamoja na wapishi wanaweza kufanya kazi na hata kiwango cha ziada cha marupuupu watakachopata.
Mageuzi hayo ya kikatiba yataanza kutekelezwa wiki ijayo wakati ambapo rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff atatia saini,mswaada huo.
Mswaada huo unaojulikana kama mswaada wa wafanyakazi wa majumbani, una uwezo wa kutikisa tamaduni za nchi hiyo kuhusiana na ajira ya wafanyakazi hao.

Kwa mara ya kwanza, sawa na wafanyakazi wengine wanaoajiriwa kwa mikataba , wafanyakazi, wa majumbani nchini Brazil wataruhusiwa kufanya kazi kwa masaa manane kwa siku na kulipwa pesa za ziada kwa masaa zaidi watakavyofanya kazi pamoja na marupurupu mengine yanayotolewa kwa wafanyakazi wengine nchini humo.
Wakati wa kipindi cha kupigia kura mswaada huo, maseneta waliutaja mswaada huo kama wa kihistoria ambayo unafutilia mbali tabia ya utumwa.
Kwa kawaida familia nyingi za kipato cha kadri nchini Brazil, huwaajiri wapishi na wafanyakazi ambao wakati mwingine wanaishi na waajiri wao.
Katika miaka ya hivi karibuni, wafanyakazi wa majumbani wamekuwa wakipewa haki wanazostahili kama kupewa likizo na pia kupewa muda wa mapumziko wakati wanapojifungua mimba.
Mabadiliko hayo huenda yakaongeza gharama ya kuwaajiri wafanyakazi wa majumbani kwa asilimia ishirini.
Kulingana na shirika la wafanyakazi duniani,Brazil ndio nchi yenye idadi kubwa ya wafanyakazi wa majumbani duniani wakiwa milioni saba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...