Language

Saturday 2 March 2013

HABARI MUHIMU: KIONGOZI WA AL-QAEDA AUAWA MALI


Kiongozi mmoja mkuu wa kundi la wapiganaji la al-Qaeda ameuawa nchini Mali. Taarifa hizi zimethibitishwa na Rais wa Chad, Idriss Deby

Alisema kuwa majeshi ya nchi yalimuua Abdelhamid Abou Zeid, wakati wa makabiliano yaliyotokea katika eneo moja la vijijini nchini Mali.
Anasemekana kuwa wa pili kwa ngazi ya uongizi
katika kundi hilo ambalo linapigana na majeshi ya kigeni nchini Mali.
Raia huo wa Algeria anatuhumiwa kwa mauaji ya mateka wawili kutoka nchi za magharibi Edwin Dyer raia muingereza mwaka 2009 Michel Germaneau raia wa ufaransa mwaka uliofuata.
Mwandishi wa BBC Thomas Fessy anasema kuwa ikiwa wataweza kuthibitisha kifo hicho, maswali bila shaka yataibuka kuhusu mateka wa Ufaransa wanaoaminika kuwa walikuwa mikononi mwa Abou Zeid.
Mwezi Januari, Ufaransa ilituma wanajeshi 3,500, Kaskazini mwa Mali, kwa lengo la kuwafurusha wanamgambo wa kiisilamu waliokuwa wameteka sehemu ya jangwa la Sahara.
Chad ni mojawapo ya nchi nyingi za Afrika ambazo zinaunga mkono harakati za jeshi la Ufaransa nchini Mali.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...