Language

Saturday 2 March 2013

HABARI MUHIMU: RAIS HUGO CHAVES HAJAFA KAMA ILIVYODAIWA


Wasaidizi wa karibu na ndugu wa rais Hugo Chavez wa Venzuela wamekanusha habari kuwa rais huyo anaweza kuwa amefariki au anakaribia kufa kutokana na ugonjwa wa saratani, na kusema kuwa bado anapigana kuokoa maisha yake.


Wasaidizi wa karibu na ndugu wa rais Hugo Chavez wa Venzuela wamepinga habari zilizosambaa kuwa rais huyo anaweza kuwa amefariki au anakaribia kufa kutokana na ugonjwa wa saratani, na kusema kuwa bado anapigana kuokoa maisha yake.

Makamu wa rais wa Venezuela Nicolas Maduro alisema siku ya Ijumaa kuwa Chavez yuko katika hali nzuri, lakini akipigania maisha yake wakati akifanyiwa tiba ya kutumia kemikali katika hospitali ya kijeshi mjini Caracas. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Maduro kutangaza kuwa rais huyo ameanza kutumia tiba hiyo ya kemikali kufuatia upasuaji wa nne wa saratani nchini Cuba mwezi Desemba, na kuamua kuendelea na matibabu nchini kwake. Alisema Chavez na madakatari wake waliamua kuanza tiba ya kemikali na mionzi, baada ya hali yake kuboreka mwezi Januari.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...