Language

Friday 8 March 2013

HABARI MUHIMU:MTU ALIYE BADILIKA KUWA ALBINO RUNGWE...STORY KAMILI IKO HAPA


MTU mmoja mkazi wa Kijiji cha Igogwe kata ya Bagamoyo wilayani Rungwe mkoani hapa amebadirika ghafra na kuwa mlemavu wa ngozi (Arbino).

Akisimulia maajabu hayo mtu huyo  Neema  Masebo (26) alisema kuwa alipatwa na mkasa huo alipokwenda kijijini kwao kuwasalimia wazazi wake akitokea nyumbani kwake jijini Mbeya.
Neema alisema kuwa Mama yake mzazi Tumaini Mlawa alipoona hali hiyo alimkimbiza katika hospital ya Wilaya ya Rungwe Makandana kwa ajili ya matibabu ambapo alilazwa siku 7 lakini hali yake ikaanza kubadirika kuwa mbaya huku ngozi yake ikianza kuchubuka taratibu hadi alipobadilika na kuwa mlemavu wa ngozi yaani (Albino).

Aliongeza kuwabaada ya madaktari kushindwa kuzuia hari hiyo isiendelee alifika Mganga wa hospitali ya serikali ya Marekani, Dr, Jescar akiwa katika ziara ya kikazi katika hospitali hiyo alimchukua vipimo na kuvituma nchini kwake kwa uchunguzi zaidi lakini hakuletewa majibu, na badala yake alipewa mafuta ya kuzuia mionzi ya jua na kuondoa vidonda, aina ya AQUASPORT LOTION, ambayo yamemsaidia kutokuwa na vidonda,
Alisema kuwa mara baada ya kupewa mafuta hayo alitoka hospital huku tayari akiwa na ulemavu huo, ndipo alipotokea mama mmoja jirani yake ambaye jina lake halikutajwa, aliyempeleka kwenye kanisa la maombi la Temple of prayer for all nations church, la wilayani Kyela, ambako alifanyiwa maombezi ikiwa ni pamoja na kupakwa mafuta ya upakona hatimaye hali yake imeanza kurejea taratibu.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Bagamoyo wilayani Rungwe wamelihusisha tukio hilo na imani za kishirikina huku wakisema kuwa toka dunia hii ilipoanza hawajawahi kuona tukio kama hilo la mtu wa kawaida kubadilika ghafra kuwa na ulemavu wa ngozi yaani Arbino.
Mchungaji wa kanisa hilo Nabii Charles Mkuvasa amekili kumpokea mgonjwa huyo kanisani kwake na kwamba alipoletwa na mama huyo alikuwa na hali mbaya lakini baada ya kumfanyia maombi na yeye kupokea uponyaji kutoka kwa yesu kristo, nakusema kuwa hali yake sasa imeanza kurejea taratibu na mungu yupo pamoja naye atarejea na kuwa kama zamani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...