Language

Saturday 13 April 2013

BARCELONA KUKUTANA NA REAL MADRID KATIKA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA PALE WEMBLEY?



Barcelona na Real Madrid zinaweza kukutana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Wembley, London Mei mwaka huu baada ya ratiba ya mechi za hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo iliyotolewa jana mchana kuzitenganisha.
Barcelona wamepangwa kucheza na Bayern Munich, wakati Real Madrid watacheza na Borussia Dortmund.
Mechi za kwanza hizo zitachezwa kati ya Aprili 23, na 24 kisha marudiano kati ya Aprili 30 na Mei. 1. Katika Ligi ya Europa, Chelsea watasafiri kwenda Uswisi kucheza na Basel Aprili 25, huku Fenerbahce wakiikabili Benfica. Mechi za marudiano zitachezwa Mei 2.
Chelsea ni timu pekee ya England iliyobaki kwenye mashindano ya Klabu Ulaya baada ya kusonga mbele kufuatia kuitoa Rubin Kazan ya Russia.
Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa, ratiba iliyotolewa jana mjini, Nyon, Uswisi, iliepusha timu Ujerumani kukutaka kwenye hatua ya nusu fainali, vilevile timu za Hispania kwenye hatua hiyo.

Real waliwatoa Galatasaray kwa jumla ya mabao 5-3, huku Barcelona waliwatoa Paris St-Germain kwa faida ya mabao ya ugenini.
Mabingwa wapya wa Bundesliga, Bayern waliwatoa Juve kwa mabao 4-0, baada ya kushinda 2-0 (nyumbani na ugenini), huku wenzao Dortmund wakiichapa Malaga 3-2

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...