Language

Friday 26 April 2013

UHURU KENYATTA ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amelitangaza baraza lake la mawaziri ambalo kwa kiasi kikubwa limeundwa na sura ngeni na wengi wao ni wasomi waliobobea kwenye fani mbalimbali.
Katika majina 16 aliyopendekeza ambayo baadaye yatafanyiwa uchunguzi na Bunge kabla ya kuidhinishwa, Rais Kenyatta amezirejesha sura mbili ambazo zilizoeleka kwenye siasa za Kenya, ambao ni Najib Balala na Charity Ngilu.

Wote kwa pamoja walikosa ubunge katika majimbo yao kwenye uchaguzi wa Machi 4, kutokana na kumuunga mkono Uhuru, lakini alisema kwamba amewaagiza kuachana na siasa ili kutekeleza majukumu yao mapya.
Balala ambaye amependekezwa kuwa Waziri wa Madini, wakati Ngilu akipendekezwa kuwa Waziri wa Nyumba na makazi, kunatazamiwa kuzusha mjadala mkubwa miongoni mwa makundi ya kijamii.
Uteuzi wa Waziri mpya wa Ulinzi, Rachel Omamo ni miongoni mwa uamuzi unaozua mjadala kuhusu uwezo wa Serikali mpya ya Kenyatta kutokana na nchi hiyo kukabiliwa na tishio kubwa la kiusalama hasa kutoka kwa wanamgambo wa Al-Shabaab wa Somalia.
Akitangaza baraza hilo la mawaziri kwa kuwaita mmojammoja na kutaja wasifu wao kisha kuwapa muda wa kuzungumza, Kenyatta alisema baraza lake litakuwa la mawaziri wanataaluma na wanasiasa watakuwa wawili tu, yaani yeye na makamu wake, Ruto.
“Tumekubaliana kwenye baraza letu kutakuwa na wanasiasa wawili tu, mimi na Makamu wa Rais William Ruto,” alisema Rais Kenyatta mara baada ya kumaliza kutangaza majina ya mawaziri hao Ikulu.
Awali Rais Kenyatta alitangaza majina manne likiwemo jina na mwanadiplomasia wa siku nyingi ambaye hivi karibuni alianzisha kampeni ya kuwania nafasi ya Ukurugenzi katika Shirika la Biashara Duniani (WTO), Amina Mohammed.
Amina amependekezwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, akiwa ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa katika nafasi hiyo tangu Kenya ijinyakulie Uhuru wake mwaka wa 1963.
Mawaziri wengine waliopendekezwa ni Adan Mohamed ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Baclays Afrika (Viwanda na Maendeleo ya Biashara), Anne Waiguru (Maendeleo ya Wananchi na Mipango), na Felix Tarus Kosgey (Kilimo, Mifugo na Uvuvi).
Wengine ni Judy Wahungu (Maji na Maliasili), Hassan Wario (Michezo na Utamaduni), Jacob Kaimenyi (Elimu), Francis Kimemia (Katibu wa Baraza la Mawaziri) na Lawrence Lenayapa (Mnadhimu wa Ikulu).
Waziri mwingine aliyeteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta kuwa katika baraza lake la mawaziri ni Henry K. Rotich, kuongoza Wizara ya Fedha. Rotich ambaye ni msomi na mchumi alifanya kazi kwa muda mrefu katika Wizara ya fedha nchini Kenya na hata katika Benki Kuu ya nchi hiy

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...