Language

Thursday 2 May 2013

HUENDA GEREZA LA GUANTANAMO LIKAFUNGWA


Katika mkutano na waandishi wa habari jana Jumanne, rais Obama alisema nchi yake haiweze kuendelea kuwaweka watu hao katika eneo lisilo katika himaya ya nchi yoyote milele.
Obama alibainisha hoja zake za kulifunga gereza hilo, akisema kuwa uendeshwaji wake umekuwa na gharama kubwa huku likikosa ufanisi, na kwamba linaathiri sifa ya Marekani katika jamii ya kimataifa, na kupunguza ushirikiano na washirika wake katika vita dhidi ya ugaidi.
Obama alisisitiza kuwa ni muhimu kuelewa kuwa Guantanamo siyo muhimu kuifanya Amerika kuendelea kuwa salama. "Wazo kwamba tutaendelea kuliweka kundi la watu ambao hawajashtakiwa kwa muda mrefu, ni kinyume na utamaduni wetu na laazima jambo hilo likome," alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...