Mwimbaji nguli wa muziki wa taarab Fatma Baraka aliyejibebea
umaarufu kwa jina la Bi Kidude ameiaga dunia mchana wa leo huko Bububu, Zanzibar.

Fatma ambaye pia ni mwimbaji wa kundi la muziki la Gusa Gusa Dar es Salaam amesema kuwa taratibu za mazishi bado
zinaendelea kufanyika wakati mwili wa marehemu unapelekwa nyumbani kwake Raha Leo.
Kutokana na taarifa tulizozipata Bi kidude amefariki akiwa na umri wa
miaka 103. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen.
No comments:
Post a Comment