Mwanamuziki mwenye makeke, Lady Gaga ameendelea kusogeza nyuma ziara ya
kutangaza muziki wake ya ‘Born This Way Ball tour’.
Rafiki wa karibu wa msanii huyo amesema kuwa amesogeza nyuma ziara hiyo
hadi Septemba mwaka huu,kutokana na hali yake kuwa bado sio nzuri.
“Yupo Chicago chini ya uangalizi wa mpenzi wake Taylor Kinney, ingawa
kwa sasa anaendelea vizuri na anaweza kutembea taratibu daktari wake amesema
bado anahitaji kupona zaidi”alisema.
Gaga amelazimika kuahirisha ziara hiyo mara mbili kutokana na kuumia
nyonga na kufanyiwa upasuaji ambapo hali yake inaendelea vizuri licha ya kuwa
bado yupo kwenye uangalizi wa madaktari.
No comments:
Post a Comment