Language

Wednesday, 17 April 2013

FIFA KUHUKUMU KESI YA MALINZI NA WENZAKE USWISI



Hatima ya wagombea sita walioenguliwa kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania, sasa itajulikana baada ya ujumbe wa Fifa kurejea Uswisi.

Wagombea ambao hatima yao ipo mikononi mwa Fifa ni Jamali Malinzi, Michael Wambura, Hamad Yahaya, Eliud Mvela, Farid Nahd na  Mbasha Matutu.
Hayo yalibainishwa na Henry Tandau wakati akiwaambia wagombea kuwa  majibu hayatatolewa hapa leo (jana), lakini hadi pale ujumbe wa Fifa chini ya Primo Cavaro watakaporejea Zurich na kupitia maelezo yote ndipo watakapotuma majibu ya suala hilo.
Awali ujumbe huo wa Fifa ulifanya kikao na sekretarieti ya TFF kuanzia asubuhi mpaka saa tano ambapo iliingia kamati ya uchaguzi chini ya Deogratius Lyato.
Wagombea sita waliokuwa kwenye viunga vya hoteli ya Serena kulipofanyika kikao hicho tangu saa tano asubuhi hadi saa tisa.
Ndipo saa kumi jioni, Tandau alipotoka na kuwatangazia wagombea kuwa wataingia wenyewe bila ya mawakili wao.

“Mtaingia wenyewe bila ya kuongozana na mawakili wenu, pia kuhusu majibu hayatatangazwa leo hadi pale ujumbe wa Fifa utakaporejea Zurich na kupitia kwa umakini ndipo watakapotoa uamuzi na kutuma.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...