Language

Thursday 28 March 2013

MSHAHARA KIMA CHA CHINI KUTANGAZWA MWEZI APRILI


Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amesema mwezi ujao wanatarajia kutangaza kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa sekta zote.

Akizungumza jana wakati wa mkutano kuhusu sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa Baraza Kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), alisema kwa muda mrefu kiwango cha kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wa sekta zote kilikuwa hakijabadilishwa.
“Kwa muda mrefu tulikuwa hatujatangaza kima cha chini cha mshahara, lakini nafurahi kuwajulisha tu kwamba mwezi ujao tutatangaza rasmi,”alisema Kabaka.
Pia alitahadharisha kuhusu utitiri wa vyama katika sehemu moja ya kazi kushauri waajiri wasiruhusu wafanyakazi waanzishe kwa sababu vitakosa nguvu ya kujadiliana na mwajiri katika kufunga mikataba ya hiyari .
Waziri huyo alisema sekta ya hifadhi ya jamii ina idadi ndogo ya wanachama waliojiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ukilinganisha na idadi ya nguvu kazi iliyopo ambayo ni milioni 22.
Awali Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Irene Isaka alisema hadi sasa michango katika mifuko hiyo imefikia Sh 1.4 trilioni na kwamba mafao yanayolipwa yamepanda kutoka Sh500 bilioni hadi kufikia Sh 724 bilioni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...