Language

Thursday 28 March 2013

SASA NI AMINI NA LINAH TENA


Kama wewe ni mpenzi wa burudani na ni mfuatiliaji mzuri wa muziki wa kizazi wa kizazi kipya hapa Tanzania basi ni lazima unawajua vizuri ESTELINA Sanga ‘Linah’ na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Amini Mwinyimkuu ‘Amini’.
Wakali hao wamenaswa katika pozi jipya la kimahaba zaidi baada ya lile busu lililoonekana katika jukwaa la fainali za EBSS mwaka jana walipokuwa wakiutambulisha wimbo uitwao ‘Mtima Wangu’.
Picha hiyo inayowaonesha wawili hao wakiwa ndani ya gari huku mwanadafada akimbusu Amini, imedakwa juzikati katika mtandao wa BBM, ambapo wadau wanaotumia mtandao huo waliwapongeza kwa kurudiana.
Baada ya mwandishi wetu kumtafuta Linah, alipopatikana alijibu kwa kifupi kwamba hana tatizo na Amini hivyo yupo huru kwa lolote mbele yake na wanafanya naye kazi kwa karibu.
Kwa upande wake Amini,  alipoulizwa juu ya ishu hiyo alitiririka: “Linah ni mtu wangu hivyo sina ubaya naye kwa kila kitu hatujawahi kugombana wala kusutana picha zisiwashtue watu,” alisema Amini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...