Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema iwapo amani
itatoweka kutokana na vurugu za kidini, watawashtaki viongozi wa CCM Mahakama
ya Kimataifa ya The Heague.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mwenyekiti wa
Chadema Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael wakati akimkaribisha Mbunge wa Moshi
Mjini, Philemon Ndesamburo kuhutubia mkutano wa hadhara.
Michael ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Moshi, alisema baadhi ya
viongozi wa Serikali ya CCM ndiyo kiini cha mbegu za chuki za kidini,
walipoituhumu Chadema kuwa ni chama cha kidini.
“Nataka niwaambie leo, amani ya Tanzania ikivurugika tunawapeleka
viongozi wote wa Serikali ya CCM The Heague, wao ndiyo chanzo cha chuki
hizi za udini ambazo zinaligawanya taifa,” alisema Michael.
No comments:
Post a Comment