Kampuni ya Uingereza ya Hawk-Eye imeshinda tenda na kupatiwa mkataba wa
kufunga vifaa maalumu kwenye viwanja vyote 20 vya timu za ligi kuu nchini
England.
Hawk-Eye itafunga kamera saba kwenye kila goli maalumu kwa kutambua
kama mpira umevuka mstari wa goli na kumjulisha mwamuzi wa mchezo huo kupitia
saa yake ya mkononi,na imesema inauhakika hakuna marejeo yoyote ya matangazo ya
picha ambayo yatapingana na maamuzi ya teknolojia hiyo.
Kampuni hiyo ya Hawk-Eye inajulikana kwa kufunga teknolojia kama hiyo
kwenye mchezo wa Tenesi na Kriketi,ambapo camera maalumu huweza kutambua iwapo
mpira umegusa mstari ama la na kumjulisha mwamuzi na wasaidizi wake ndani ya
sekunde chache.
Chama cha soka nchini England FA,kitafunga vifaa hivyo kwenye uwanja wa
Wembley tayari kwa kutumika kwenye mchezo wa ngao ya jamii hapo mwezi wa nane
mwaka huu.
Vilabu vikubwa vyote nchini England vimepiga kura ya kupitisha maamuzi
hayo katika mkutano wao uliofanyika hii leo jijini London,Huku viwanja vingine
vya timu 17 zitakazosalia ligi kuu na zile 3 zitakazopanda daraja vitawekewa
teknolojia hiyo na shughuli nzima itachukua wiki sita kukamilika.
Msukumo wa kutumia teknolojia maalumu ya kutambua goli ilipata nguvu
baada England kukataliwa goli lao la kusawazisha walipocheza na Ukraine,Mchezo
ambao England walifungwa bao moja kwa bila kwenye michuano ya kombe la mataifa
barani Ulaya mwaka 2012, Ambapo mwezi mmoja baadaye bodi ya vyama vya soka vya
kimataifa (IFAB) katika kikao chake mjini Zurich kilipitisha teknolojia mbili
ili zitumike kwenye michezo ya soka.
Nalo shirikisho la kandanda Ulimwenguni FIFA kupitia kwa rais wake Sepp
Blater alisema kukataliwa kwa goli la Frank Lampard kwenye mechi ya robo
fainali kati ya England na Ujerumani mwaka 2010 katika michuano ya kombe la
dunia,kulichangia kwa kiasi kikubwa maamuzi ya shirikisho hilo kupitisha sheria
ya matumizi ya teknolojia ya kutambua goli.
Chama cha soka cha England kimesema kingependa kuona teknolojia hiyo
inaanza kutumika kwa vitendo haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment