Watoto ni wahanga wakubwa wa udhalilishaji wa kingono katika maeneo ya
mizozo, linalalamika shirika la Uingereza, Save the Children na kuutaja utovu
huo kuwa 'maovu makubwa na ya kutisha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo lisilomilikiwa na serikali, Save
The Children, iliyochapishwa jana mjini London, zaidi ya asilimia 70 ya wahanga
wa ubakaji katika nchi zilizoathirika zaidi na vita, mfano wa Liberia au Sierra
Leone, ni watoto.
Uchunguzi uliofanywa umebainisha kwamba watoto wenye umri wa miaka
miwili waliangukia mhanga wa visa vya kinyama vya maprofesa, wakuu wa kidini na
wanajeshi waliopelekwa kwa ajili ya kutumikia harakati za kusimamia amani.
Uchunguzi huo unazungumzia pia kuhusu vifo vya watoto walioangukia mhanga wa
ubakaji au kudhalilishwa kingono na makundi ya wanajeshi.
"Inashtusha kuona idadi ya watoto walioangukia mhanga wa visa vya
udhalilishaji wa kingono katika maeneo ya mizozo, ikifikia kiwango cha kutisha
kama hicho," amesema Justin Forsyth, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa shirika
hilo la Save The Children. "Visa vya kuwadhalilisha watoto kingono ni
mojawapo ya ushenzi mkubwa na uliofichika wa vita," ameshadidia mkurugenzi
huyo.
No comments:
Post a Comment